Baada ya mechi ya jana, Kessy na Chirwa wawakuna Wazambia huku mipango ya kuwanasa ikianza namna hii
Majina ya wachezaji wawili wa Yanga, beki Hassan Ramadhan 'Kessy' na Obrey Chirwa yamepata umaarufu mkubwa muda mfupi bada ya kumalizika kwa pambano kali kati ya Yanga na Zanaco lililopigwa jana.
Wachezaji hao walionyesha uwezo mkubwa katika mchezo huo kiasi cha kuwashawishi makocha wa timu mbalimbali za jijini Lusaka kuandika majina yao tayari kwa kuwapa dili la kucheza soka endapo mipango ikikaa sawa hapo baadae.
Aliyekuwa kocha wa Simba, Mzambia Patrick Phiri ambaye kwa sasa anainoa timu ya Rocana United, ndiye anayetumiwa kuwaunganisha viongozi wa timu na wachezaji hao.
Phiri amlifunguka kwamba katika kipindi cha mapumziko ya mchezo huo uliomalizika huku timu hizo zikitoka suluhu, alifuatwa na makocha na viongozi wa timu mbalimbali katika kujua majina ya wachezaji na pia kuulizia uwezekano wa kusajili mchezaji kutoka klabu ya Yanga.
Baada ya mechi ya jana, Kessy na Chirwa wawakuna Wazambia huku mipango ya kuwanasa ikianza namna hii
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 19, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment