Yanga katika mipango ya kumnasa mlinda mlango kutoka klabu hii...
Yanga siku zote wakiamua jambo lao hakuna wa kuwazuia na hii ni baada ya kuanza mikakati ya kuinasa saini ya kipa wa African Lyon, Mcameroon Youthe Rostand ambaye anatoka nchi moja na kocha wa Simba Joseph Omog.
Kipa huyo ameonyesha kiwango kizuri katika timu yake hiyo hali iliyoufanya uongozi wa Yanga kushawishika kumuhitaji katika usajili wao wa msimu mpya 2017/18.
Yanga inahitaji kufanya usajili mzuri msimu ujao na sehemu ambayo wanataka kuanza nayo ni kipa ambaye ataungana na Deo Munishi pamoja na Ally Mustafa.
Taarifa za uhakika kutoka kwa rafiki wa karibu wa kipa huyo, zinadai kuwa tayari uongozi wa klabu hiyo umempa jukumu kigogo mkubwa wa timu hiyo kuzungumza na kipa huyo kwa ajili ya kusaini mkataba na kwa jinsi mambo yanavyokwenda kila kitu kitakamilika kwa muda.
"Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, tayari makubaliano yameshafanyika kwani kigogo mmoja amejitolea kwa kipindi hiki kumlipia baadhi ya huduma ikiwemo mazoezi ya gym pamoja na kumpa pesa za kumsaidia," alisema.
Yanga katika mipango ya kumnasa mlinda mlango kutoka klabu hii...
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 19, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment