Mama yake Lukaku atupiwa lawama na Everton, Klopp macho kwa Dembele...hizi hapa tetesi za usajili magazeti ya Ulaya Jumapili hii
Everton wanamlaumu mama wa Romelu Lukaku kwa kuchangia mwanae kutaka kuihama klabu hiyo.
Nyota huyo Mbelgiji mwanzoni alionesha nia ya kutaka mkataba mpya lakini amebadili mawazo yake ghafla.
Inatizamiwa majira ya joto nyota huyo mkali wa kutupia anaweza kuondoka Goodison Park huku gazeti la The Times likidai mama yake ni wa kutupiwa lawama juu ya swala hili.
Ukiachana na Lukaku, pia kuna hizi nyingine magazeti ya Ulaya leo kuhusu usajili
- Arsenal nao kuingia katika harakati za kumnasa Ross Barkley endapo Everton wataamua kumuuza msimu huu, Chelsea na Tottenham hawapo mbali kuisaka saini hiyo.
- Chelsea wanaandaa kiasi cha pauni mil 40 kuwasajili kwa mkupuo Benjamin Mendy and Bernardo Silva kutoka Monaco.
- Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp anajipanga kumnasa Ousmane Dembele kutoka Borussia Dortmund majira ya joto huku Barcelona pia wakimvizia.
- Huenda Steven Gerard akawa mrithi wa kiti cha kocha wa sasa Liverpool, Jurgen Klopp kwa baadae .
- Liverpool kutenga kiasi cha pauni mil 35 kwa ajili ya beki wa kati wa Roma, Kostas Manolas.
- Tottenham wanataka kusikia jibu moja tu kutoka kwa Real Madrid, kwamba endapo watamuuza kiungo Mateo Kovacic katika majira ya joto.
- Ryan Sessegnon amepuuza ofa kutoka Liverpool baada ya kuamua kuongeza mkataba mwingine katika klabu ya Fulham.
- Tottenham wapo tayari kumsajili mshambuliaji kutoka Real Betis, Antonio Sanabria.
Mama yake Lukaku atupiwa lawama na Everton, Klopp macho kwa Dembele...hizi hapa tetesi za usajili magazeti ya Ulaya Jumapili hii
Reviewed by Steve
on
Sunday, March 19, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment