Man City bado wanamtaka Messi, Wenger agoma kuondoka, hizi hapa tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo
Manchester United huenda wakatapata upinzani mkubwa endapo wakitaka kumsajili beki wa kulia wa Benfica, Nelson Semedo.
Kwa mujibu wa Ojogo, miongoni mwa vilabu vikubwa Ulaya, Juventus na AC Milan vimeonesha nia ya kumtaka beki huyo Mreno.
Pia Barcelona, Bayern Munich na Inter Milan ni miongoni mwa vilabu vinavyotajwa sana kutaka kunasa saini ya Mreno huyo.
Pia kuna habari nyingine za leo zilizotawala magazetini Ulaya kuhusu usajili leo
- Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amechukua maamuzi ya kutaka kuendelea kukaa klabuni ambapo atakua na maongezi na bodi ya klabu.
- Katika kutaka kuziba pengo la Andres Iniesta, Barcelona wanawafukuzia Phillipe Coutinho wa Liverpool na Marco Verratti kutoka PSG.
- Miongoni mwa wachezaji wanaopewa kipaumbele katika usajili kikosi cha Spurs, ni kiungo mkabaji wa zamani wa Liverpool, Suso.
- Manchester City bado wanamfuatilia kwa karibu Mahmoud Dahoud wa Borussia Monchengladbach.
- Chelsea wanaamini kwamba wapo katika nafasi nzuri kumnasa kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko.
- Barcelona wapo katika mpango wa kumnasa 'Neymar' mwingine, mchezaji wa kikosi cha Brazil wachezaji chini ya miaka 17, winga Vinicius Junior ambaye pia amevivutia vilabu vya Real Madrid, Arsenal na Chelsea.
- Man City wanaamini kwamba wanaweza kumleta Etihad mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ulimwenguni mara tano, Lionel Messi.
- Aliyewahi kua kocha wa Italia, Cesare Prandelli ameamua kuitosa ofa ya Leicester baada ya kutoridhishwa na klabu hiyo inavyomtendea kocha wao wa sasa, Claudio Ranieri.
Man City bado wanamtaka Messi, Wenger agoma kuondoka, hizi hapa tetesi za usajili magazeti ya Ulaya leo
Reviewed by Steve
on
Monday, March 20, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment