Hawa ndio nyota kutoka Yanga ambao Pluijm ana mpango wa kuwavutia Singida United
Kuna uwezekano mkubwa wa kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm, akazua kizaazaa kwenye klabu hiyo, kutokana na mpango wake wa kutaka kuwang'oa nyota kadhaa kuungana nao kwenye timu yake mpya ya Singida United.
Wachezaji wanaodaiwa kusakwa na Pluijm ni pamoja na kiungo wa kati wa klabu hiyo, Thabani Kamusoko, mshambuliaji Donald Ngoma na winga Simon Msuva.
Habari za ndani kutoka kwenye timu ya Singida, zinasema kocha huyo amependekeza majina ya wachezaji kadhaa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara, ambapo wachezaji hao ni nyota kadhaa wa Yanga pamoja na mshambuliaji wa Ndanda FC, Atupele Green.
"Kama inavyojulikana kuwa Pluijm ndiye aliyefanikisha usajili wa wachezaji kama Kamusoko na Ngoma, hivyo anaweza kuwashawishi wakaungana naye baada ya msimu huu kumalizika. Pia wachezaji wenyewe watakuwa wamemaliza mikataba yao," kilieleza chanzo cha taarifa.
Hawa ndio nyota kutoka Yanga ambao Pluijm ana mpango wa kuwavutia Singida United
Reviewed by Steve
on
Monday, March 20, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment