Msuva akiri wazi kukosekana kwa Tambwe na Ngoma lilikuwa pigo kubwa Ligi ya Mabingwa
Winga wa Yanga, Simon Msuva amesema kukosekana kwa washambuliaji Amis Tambwe na Donald Ngoma katika kikosi chao kumesababisha kuondolewa mapema Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ngoma alishindwa kucheza mchezo wa marudiano uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mashujaa, Lusaka na Tambwe alikosa mechi zote mbili dhidi ya Zanaco ya Zambia, kutokana na kuwa majeruhi, hivyo Wanajangwani hao kuaga kwenye michuano hiyo.
Msuva amefunguka kwamba Tambwe na Ngoma ni washambuliaji muhimu katika kikosi caho, kwani kukosekana kwao kumewafanya watolewe mapema Ligi ya Mabingwa.
"Kila mchezaji ana umuhimu wake katika timu, tukubali au tukatae, tuna kikosi kipana, lakini hawa jamaa wawili ni muhimu sana kwetu," alisema Msuva.
Msuva akiri wazi kukosekana kwa Tambwe na Ngoma lilikuwa pigo kubwa Ligi ya Mabingwa
Reviewed by Steve
on
Monday, March 20, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment