Mechi sita za Simba zilizosalia, Omog amekuwa na mipango hii...
Kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon anazidi kukuna kichwa kuhakikisha anazitumia vema mechi sita zilizosalia katika Ligi kuu Bara.
Simb kwa sasa inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 55, katika mechi hizo sita za kumaliza msimu, imebakiza kucheza mechi dhidi ya Kagera Sugar, Toto Africans, Mbao FC, Mwadui, Stand United na Prisons.
"Tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha tunakuwa mabingwa msimu huu kwani hicho ndicho kinachosubiriwa kwa hamu kubwa klabuni hapa na hatupo tayari kuona tunakosa ubingwa.
"Tumebakiwa na mechi sita kumaliza msimu, wapo watu wanaosema kuna baadhi ya mechi ni nyepesi, kitu ambacho kwangu hakiniingii akilini.
"Naweza kusema tuna mechi ngumu tena zaidi ya zile tulizowahi kucheza huko nyuma, hatuwezi kudharau hata kidogo timu tutakazocheza nazo, ni lazima tuziheshimu ili kupata matokeo mazuri," alisema Omog.
Mechi sita za Simba zilizosalia, Omog amekuwa na mipango hii...
Reviewed by Steve
on
Monday, March 20, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment