Tetesi: Man United wana mpango na Guardiola
Imeripotiwa kua klabu ya Manchester United ina mpango wa
kumleta Pep Guardiola Old Trafford mwaka 2016 pamoja na kwamba kocha wa sasa, Louis van Gaal anaonekana kutaka kumpokeza kijiti msaidizi wake, Ryan Giggs.
Inadaiwa kua kocha huyo wa Bayern Munich yuko tayari kuondoka Allianz Arena msimu ujao huku Man City nao wakionesha nia ya kumpata.
Van Gaal ambaye mara kadhaa amenukuliwa kua na mpango wa kustaafu mwaka 2017 ameripotiwa kutaka kumrithisha kiti hicho Ryan Giggs, lakini sasa kwa mujibu wa The Mirror klabu inamtaka Guardiola.
Endapo Guardiola ataamua kuondoka Bayern msimu ujao, kocha Van Gaal atakua amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake itafahamika sasa endapo Man United watamchukua au la.
Kocha huyo mhispania amepata kuchukua mataji mawili ya klabu bingwa yote akiwa na Barcelona na pia ameiwezesha Bayern kuchukua mataji mawili ya Bundesliga.
Tetesi: Man United wana mpango na Guardiola
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 20, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 20, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment