Mourinho: Nitaionesha dunia Falcao ni nani!!
Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho amewatoa shaka mashabiki wa soka kua Radamel Falcao bado anaweza kama
akipata nafasi ya kufanya nae kazi.
Chelsea katika mazungumzo na Falcao
Mshambuliaji huyo kwa sasa yupo klabuni kwake Monaco baada ya kuichezea Man United msimu uliopita na kwa kiasi kikubwa amekua akihusishwa na kuhamia Stamford Bridge.
Alipokua akiongea na South American Tv, Mourinho aligusia kua ana nia ya kutaka kufanya kazi na Falcao na anaumia jinsi mashabiki nchini Uingereza wanavyomchukulia Falcao kirahisi.
"Nitamsaidia Falcao kurudi kiwango chake tena, ninaweza" alimwambia ripota, kama ilivyonukuliwa na Daily mail.
"Inaniumiza kuona kua mashabiki Uingereza wakifikiria kua Falcao wa ukweli ni yule waliyemuona pale Manchester United."
Falcao yupo Chile na kikosi cha timu yake ya taifa ya Colombia kwa ajili ya michuano ya Copa america inayoanza leo.
Mourinho: Nitaionesha dunia Falcao ni nani!!
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
