Messi ataja timu mbili anazopenda kuziangalia.
Nyota wa FC Barcelona, Lionel Messi, ametaja timu mbili nje ya La liga ambazo anapenda kuzitazama
uwanjani.
Soma: Messi ataja watatu anaoogopa kukutana nao
Utashangaa kua Messi aliyeshinda vikombe vitatu msimu huu akiwa na klabu yake, amewataja wakali kutoka Ujerumani, Bayern Munich kua ni timu anayoipenda ukitoa timu anayoichezea sasa.
"Pep anafanya makubwa na Bayern Munich na anatengeneza timu kama aliyokua nayo Barcelona, lakini ikiwa na wachezaji tofauti na tofauti zingine kidogo" aliiambia Squawka.
"Kila mara anajitahidi kufanya vitu vipya, na hicho ni kitu kizuri katika mchezo wa mpira."
"Tunahitaji ushindani mkubwa ndani ya Ulaya, kwa hiyo nina furaha kua Pep anatengeneza upande ambao utaleta ushindani kwa timu za La liga"
Pia Messi aliwataja wapinzani wao katika mechi iliyopita ya fainali kua ni miongoni mwa timu anazopenda kuzitizama.
"Juventus pia wamefanya makubwa msimu huu, na huwezi kuzidharau timu za Italia"
"Italia wametawala soka la ulaya kwa miaka mingi, ni wakati huu tu mambo yamekua magumu, lakini bado wanaweza kuleta ushindani"
Messi ataja timu mbili anazopenda kuziangalia.
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 11, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, June 11, 2015
Rating:
