Lionel Messi: Ronaldo si adui yangu.
Nyota wa Barca, Lionel Messi amesisitiza kua mkali mwenzie Cristiano Ronaldo si adui yake, na uhasimu kati yao uliletwa na
vyombo vya habari.
Muarjentina huyo na Mreno Cristiano wamekua na 'ka-ushindani' katika rekodi mbali mbali,-huyu anaweka hii na huyu hii, tangu mwaka 2009 Ronaldo alipoingia Real Madrid.
Hata hivyo Messi amesisitiza kua hawana ushindani, ila kila mmoja anajitahidi kufanya makubwa kwa ajili ya klabu yake.
"hakuna uhasama" Messi aliiambia Shortlist.
"Ni kitu ambacho vyombo vya habari vimeleta.
"Wote tunataka kufanya makubwa kwa vilabu vyetu na sio Ronaldo vs Messi, haijawahi kua."
Mastaa hao wamevuta hisi za mashabiki kwa sana tangu Ronaldo ahamie Real Madrid kwa dau la pauni mil. 94.
Tangu mwaka 2009, Messi ameifungia klabu yake magoli 332, wakati Ronaldo akiwa na magoli 313, kwa kuongezea Messi ametoa usaidizi katika magoli 119 , Ronaldo akitoa mara 90.
Lionel Messi: Ronaldo si adui yangu.
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
