Propellerads

Sio mashabiki tu, hata Niyonzima hili la kufungwa linamuumiza sana tu namna hii




Kiungo wa Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima ameweka wazi kwamba
ni muda mwingi amekua akiwaza ni kwa namna gani walipoteza mchezo wao dhidi ya Simba Jumamosi kwa mabao 2-1.

Katika mchezo huo ambapo Niyonzima alikua nahodha, amefunguka kwamba tangu kumalizika kwa mchezo huo amekuwa na mawazo mengi sana juu ya timu yake kama itakuwa na uwezo wa kutetea ubingwa wao wa ligi.

"Tangu siku ile nimekuwa nikiwaza ni kwa namna gani tunaweza kushinda mechi zetu zilizosalia ili tuweze kutetea ubingwa wetu wa ligi tuliouchukua msimu uliopita.

"Najua uwezo wa kupambana tunao, kuhakikisha tunatimiza malengo yetu, lakini kama hatutakuwa pamoja, hatuwezi kufanikisha hilo, hicho ndicho kinanifanya niwaze sana.

"Kama hakutakuwa na hujuma zozote dhidi yetu hakika tutashinda kila mchezo hadi mwisho kwa sababu kila mmoja aliyecheza siku ile aliumia na hakuna atakayekuwa tayari kuona tunafungwa tena," alisema Niyonzima.




Sio mashabiki tu, hata Niyonzima hili la kufungwa linamuumiza sana tu namna hii Sio mashabiki tu, hata Niyonzima hili la kufungwa linamuumiza sana tu namna hii Reviewed by Steve on Wednesday, March 01, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.