Propellerads

Daktari aanika nje ndani swala la Donald Ngoma kutocheza




Kufuatia mshambuliaji wa Yanga, Donalda Ngoma kumuita daktari
aliyemtibu kua ni 'daktari feki' katika ujumbe wake mitandao ya kijamii, daktari huyo wa zamani wa Yanga, Haroun Ali ameamua kuuanika ukweli wote juu ya swala la Ngoma kutocheza.

Awali kulikua na taarifa kwamba mchezaji huyo Mzambia alikua akisumbuliwa na majeraha hivyo kushindwa kucheza michezo kadhaa akiwemo ule ambao Yanga walikutana na Simba na kuambulia kichapo cha 2-1.

Haroun ameamua kueleza kila kitu juu ya ishu hiyo baada ya Ngoma kudai kua daktari huyo alitoa ripoti ya uongo.

"Ngoma alipaswa kusema ukweli, nimeshangazwa sana na shutuma zake za kunidhalilisha, nimemtibu na amepona lakini alitaka niandike taarifa kwamba bado anaumwa, hii ni kinyume na maadili ya kazi yangu, nilipomuuliza kwanini nifanye hivyo akasema anawadai Yanga pesa na hakuna anayemjali. Nikamwambia hilo liko nje ya uwezo wangu, nikaandika ripoti kutokana na hali halisi na alikua fiti kucheza," alisisitiza Dk. Haroun.
Daktari aanika nje ndani swala la Donald Ngoma kutocheza Daktari aanika nje ndani swala la Donald Ngoma kutocheza Reviewed by Steve on Thursday, March 02, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.