Blagnon arejea Msimbazi huku sababu kubwa ikitajwa na Kaburu
Aliyekua mshambuliaji wa Simba, raia wa Ivory Coast, Frederic Blagnon ambaye aliondolewa katika timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo mwaka huu, amerejea klabuni hapo na leo Jumatatu anatarajia kujiunga na kikosi cha timu hiyo jijini Arusha kwa ajili ya kuanza kukitumikia katika mechi za Ligi Kuu bara pamoja na Kombe la FA.
Simba ilimtoa kwa mkopo mshambuliaji huyo kwenda katika moja ya timu za nchini Oman baada ya kushindwa kukidhi matakwa ya kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog.
Hata hivyo, baada ya kufika nchini Oman mambo hayakuwa sawa kama ilivyotarajiwa na kurejea Bongo kuendelea na majukumu yake ya kuitumikia Simba ambayo ilimsajili kwa kitita cha Sh milioni 100, mwanzoni mwa msimu huu.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu' amesema sababu kubwa iliyomfanya mchezaji huyo arudi klabuni hapo ni hati yake ya uhamisho wa kimataifa (UTC) kuchelewa kufika katika klabu hiyo waliyokuwa wamempeleka kwa mkopo.
"Ni kweli kabisa Blagnon amerejea nchini na kesho (leo) Mungu akipenda atajiunga na timu jijini Arusha ambako itapiga kambi ya kujiandaa na mchezo wetu wa kombe la FA dhidi ya Madini FC ya jijini humo utakaochezwa Jumapili na baada ya hapo ataendelea kuitumikia timu yetu katika mechi zetu za Ligi kuu Bara.
"Kama ilivyokua ikifahamika kuwa Blagnon tulimtoa kwa mkopo katika timu moja ya nchini Oman, ni kweli kabisa tulifanya hivyo lakini amerejea baada ya kukosa ITC ambayo TFF walichelewa kuituma, hivyo klabu hiyo ikaona ni vyema arudi aendelee kuitumikia klabu yetu na atarudi aendelee kuitumikia klabu yetu na atarudi huko baada ya msimu kumalizika.
"Hakuna jambo lingine zaidi ya hilo lililosababisha arudi hapa nchini hapa nchini, kwani alipofika katika klabu hiyo alifanyiwa majaribio ambayo alifuzu vipimo vya afya ila tatizo ikawa ni ITC yake ambayo ilikwama TFF," alisema Kaburu.

Reviewed by Steve
on
Monday, March 13, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment