Propellerads

Endapo Simba wakichukua ubingwa ,Mo aandaa bonge la 'sapraizi' kwa wachezaji



Simba wanazidi kuzifaidi pesa za bilionea kijana, Mohamed Dewji 'Mo' ambaye
hadi mwezi uliopita ilidaiwa alikuwa ameshamwaga kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya mshahara na marurupu mengine.

Sasa Mo ameibuka na kali nyingine, amewatangazia wachezaji wa timu hiyo kuwa kama wakiutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, wajiandae kushangazwa na 'mpunga' atakaowamwagia, ingawa hakutaka kuwatajia kiasi zaidi ya kusisitiza watashangaa.

Mo amekuwa akitoa mamilioni kwa wachezaji, benchi la ufundi, mpaka madereva kila Simba inaposhinda.

Kigogo mmoja kutoka ndani ya Simba ambaye hakutaka jina jina lake kutajwa, amesema kuwa tajiri huyo amewaahidi donge nono wachezaji tofauti na fedha ambazo wanapewa kila wakishinda mechi ili kuhakikisha wanafanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu.

"Mo amewataka wachezaji wajitume kupita kiasi katika mechi hizi zilizobaki ili kuweza kutwaa ubingwa msimu huu na amewaandalia donge nono ambapo hakutaka kuliweka wazi kwa sasa na amewaambia watafurahi wenyewe mara baada ya kufanikisha hilo.

"Yaani iwe isiwe lazima tuchukue ubingwa, tumejipnga vizuri katika mechi za mwisho ili kuweza kushinda kwa kutopoteza nafasi tuliyonayo hivi sasa, hivyo kila mchezaji kwa sasa yupo na ari kuona wanafanikiwa kushinda katika mechi zote," alisema kigogo huyo.
Endapo Simba wakichukua ubingwa ,Mo aandaa bonge la 'sapraizi' kwa wachezaji Endapo Simba wakichukua ubingwa ,Mo aandaa bonge la 'sapraizi' kwa wachezaji Reviewed by Steve on Monday, March 13, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.