Propellerads

Tathmini ya Bossou kuhusu mechi ya Zanaco, afafanua makosa ya kocha Lwandamina



Beki kisiki wa Yanga, Mtogo, Vincent Bossou, amefunguk
a kuwa miongoni mwa vitu vilivyochangia wao kupata sare ya bao 1-1 mbele ya Zanaco ni kocha wao George Lwandamina kushindwa kutumia vizuri mabadiliko ya wachezaji 'sub' ambapo wachezaji wengi ambao aliwaingiza hawakuwa na msaada katika mchezo huo.

Bossou amesema kwamba hakuridhishwa na 'sub' alizofanya kocha huyo ambazo wachezaji walioingia hawakuwa na msaada wowote kwenye mechi hiyo na kuwaruhusu wapinzani wao watawale na kurudisha bao.

"Mechi ilikuwa nzuri na kila mtu aliona kwamba tulipambana kwa ajili ya kupata matokeo hapa nyumbani lakini haikuwa bahati yetu na kujikuta tukipata sare lakini ikumbukwe kwamba nao Zanaco walikuja kupata matokeo wakiwa ugenini.

"Kikubwa kilichotuponza sisi ni kuanzia eneo la viungo ambalo lilikata mawasiliano na kuwaruhusu wapinzani wetu wacheze vile wnavyotaka na kutufanya sisi mabeki tuwe na muda mwingi wa kuondoa mashambulizi kwa muda mwingi.

"Ila pia kocha Lwandamina alichemka kwa jinsi ambavyo alifanya mabadiliko ya wachezaji 'sub' kwani aliwatoa wenye uzoefu na mashindano haya na kuwaingiza wale ambao hawana hata uzoefu na kusababisha timu kufa na hilo kuchukuliwa kama faida na wenzetu," alisema Bossou.

Lwandamina alifanya sub kwa kuwatoa wachezaji Donald Ngoma nafasi yake ilichukuliwa na Emmanuel Martin, Thabani Kamusoko aliyetoka na kuingia Juma Mahadhi pamoja na Justine Zulu ambaye aliingia Deus Kaseke.
Tathmini ya Bossou kuhusu mechi ya Zanaco, afafanua makosa ya kocha Lwandamina Tathmini ya Bossou kuhusu mechi ya Zanaco, afafanua makosa ya kocha Lwandamina Reviewed by Steve on Monday, March 13, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.