Msuva adokeza kuondoka Jangwani, wapi anaelekea sasa?!....kafunguka hapa
Winga machachari na tegemeo wa Yanga, Simon Msuva,
amesema ana maisha mafupi ya kuendelea kuwepo katika timu hiyo huku akiendelea kuweka mipango yake ya kuondoka Jangwani.
Kauli hiyo aliitoa mara baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumalizika kati ya Yanga na Zanaco ya Zambia iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na matokeo kumalizika kwa sare ya 1-1.
Msuva mpaka sasa amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa kuendelea kuichezea timu hiyo inayofundishwa na Mzambia, George Lwandamina.
Kwa sasa Msuva amedai kwamba ana malengo na ndoto nyingi za kucheza soka la kulipwa, hivyo hategemei kukaa muda mrefu Yanga, huku ikiwa ni mapema kwake yeye kuweka wazi katika kipindi hiki ambacho bado ana mkataba na Yanga, kila kitu atakiweka wazi mara baada ya mkataba wake kumalizika.
Amesema pia ana ofa nyingi amezipata ndani na nje ya nchi ambazo kwa sasa amezifanya siri huku akiendelea na majukumu mengine ya kuipambania timu yake.
"Hivi unavyotegemea mimi nitaichezea Yanga milele? Hapana, nina mipango mingi niliyoweka mara baada ya mkataba wangu wa mwaka mmoja kumalizika.
"Nisingependa kuweka wazi kila kitu changu ninachokifanya katika kipindi hiki, zipo ofa nyingi lakini huu si muda wake, kwani nimebakisha mwaka mmoja wa kuendelea kuichezea Yanga.
"Bado ninaendelea kuipenda timu yangu ya Yanga inayoniajiri na kunilipa mshahara mzuri, lakini ijulikane kuwa mimi siatichezea Yanga milele," alisema Msuva.
Msuva adokeza kuondoka Jangwani, wapi anaelekea sasa?!....kafunguka hapa
Reviewed by Steve
on
Monday, March 13, 2017
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, March 13, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment