Propellerads

Mfungaji wa Zanaco anawakubali Simba na Yanga, ila anatamani zaidi achezee hapa



Mshambuliaji wa Zanaco ya Zambia, Kwame Attrams, raia wa Ghana amesema anatamani siku moja kuja kukipiga Simba.

Attrams ndiye aliyeisawazishia Zanaco baada ya Yanga kutangulia kufungwa wakati walipotoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa Jijini Dar.

Attrams amesema akizichezea Simba au Yanga inaweza kuwa njia ya kwenda kusakata kabumbu Ulaya.

Amedai atakuwa tayari kuichezea Simba kwa kuwa ni timu kongwe na zinafuatiliwa na mashabiki wengi barani Afrika ikiwamo nchini Ghana.

Straika huyo aliyeichezea timu za Groupe Sportive Bazano ya DRC Congo na Wadi Degla ya Misri, alisema malengo yake ni kutaka kuona siku moja anacheza soka Tanzania katika klabu hizo mbili zenye historia kubwa.

"Simba na Yanga ni timu kubwa, nimeanza kuzisikia tangu nikiwa mdogo natamani siku moja na mimi nije Tanzania kufanya kazi na moja ya klabu hizi," alisema Attrams.

Alisema anajisikia furaha kuifunga Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na tayari ameingia katika historia ya kuwatungua Wanajangwani hao.

Attrams alisema atajisikia zaidi akicheza pamoja na Waghana wenzake wanaokipiga Simba, James Kotei na Danieli Agyei.
Mfungaji wa Zanaco anawakubali Simba na Yanga, ila anatamani zaidi achezee hapa Mfungaji wa Zanaco anawakubali Simba na Yanga, ila anatamani zaidi achezee hapa Reviewed by Steve on Monday, March 13, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.