Propellerads

Mourinho aamua kuwajibu namna hii mashabiki wa Chelsea waliokua wakimzomea



Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amewajibu kwa ishara mashabiki wa Chelsea baada ya kumzomea jana kwenye mechi ya robo fainali ya FA jana usiku Stamford Bridge.

Kocha huyo Mreno alikuwa kipenzi kikubwa cha mashabiki wa Chelsea baada ya kufundisha kwa mafanikio makubwa klabuni hapo kwa muda wa miaka mitano katika vipindi viwili tofauti.

Lakini kwa sasa hali inaonekana kubadilika kwani tangu aanze kuinoa klabu ambayo ni hasimu mkubwa wa Chelsea katika Premier League amekua akichukuliwa tofauti na hilo limeweza kushuhudiwa jana.

Kwa mujibu wa ripoti mbali mbali katika mtandao wa Twitter, katikati ya kipindi cha kwanza, mashabiki wa Chelsea waliimba nyimbo za kumkashifu Mourinho lakini meneja huyo aliwajibu kwa kunyoosha vidole vitatu akiwa na maana kwamba aliwasaidia kuchukua mataji matatu ya Premier League kipindi akiinoa klabu hiyo.

United walijikuta wakicheza 10 pekee uwanjani baada ya Ander Herrera kutolewa nje dakika ya 35 kwa kupewa kadi ya pili ya njano.
Mourinho aamua kuwajibu namna hii mashabiki wa Chelsea waliokua wakimzomea Mourinho aamua kuwajibu namna hii mashabiki wa Chelsea waliokua wakimzomea Reviewed by Steve on Tuesday, March 14, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.