Propellerads

Kurejea kwa Jjuuko kumeacha maswali mengi ya kujiuliza




Wakati Simba wakiwa na furaha kurejea kwa beki wao kisiki,
Juuko Murshid imezuka hali ya sintofahamu miongoni mwa mashabiki kuhusu nani atakuwa kikosi cha kwanza kati ya Mganda huyo, Method Mwanjali, na Abdi Banda.

Wachezaji wote hao wapo katika nafasi moja ya beki wa kati kwa hiyo italazimu mmoja abaki benchi sasa maswali yanaibuka ni nani ataanzishwa benchi kwani wote wana uwezo mkubwa.

Jjuuko alikua nchini kwao Uganda baada ya kumalizika kwa michuano ya Afcon, na sasa amewasili kikosini akiungana na Mwanjali na Banda kupambana kwa ajili ya namba.

Kipindi Jjuuko hayupo, Banda na Mwanjali walitengeneza kombinesheni nzuri lakini ujio wake unamfanya kocha Omog kuanza kuumiza kichwa kwamba atumie njia gani kuwapa nafasi wote watatu ikizingatiwa kuwa Jjuuko naye ni mpambanaji.


Kurejea kwa Jjuuko kumeacha maswali mengi ya kujiuliza Kurejea kwa Jjuuko kumeacha maswali mengi ya kujiuliza Reviewed by Steve on Thursday, March 02, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.