Propellerads

Endapo ikibainika, Adhabu hii kumkabili Banda


Beki wa kati wa Simba, Abdi Banda yupo katika hatari ya kufungiwa

mechi tatu na faini ya shilingi laki tano endapo akikutwa na kosa la kumpiga kiwiko kiungo wa Yanga, Said Juma Makapu kwenye mchezo kati ya Simba na Yanga wikiendi hii.

Kulingana na kanuni za Ligi kuu Bara za msimu huu, kanuni ya 37 sura ya 11 kifungu cha 7 (f), ambacho ni udhibiti wa wachezaji, kufanya kitendo kitakachobainika kuwa ni kinyume na maadili ya mchezo wa mpira wa miguu, adhabu yake ni kutozwa faini isiyopungua Sh 500,000 na kufungiwa kucheza mechi zisizopungua tatu.

Ofisa Habari wa Shirikiso la soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas amefunguka kwamba mambo yote kuhusu mchezo huo yatajadiliwa leo Jumatano na kamati ya saa 72 na kama kunatukio lolote likibainika mhusika atachukuliwa hatua.

"Kamati ya saa 72 itakaa kesho Jumatano (leo) ili kuuangalia kwa kina mchezo huo na kama kutabainika kuna tukio lisilo la kawaida basi kanuni zipo zitafuatwa kuona nini kifanyike." alisema Lucas.
Endapo ikibainika, Adhabu hii kumkabili Banda Endapo ikibainika, Adhabu hii kumkabili Banda Reviewed by Steve on Wednesday, March 01, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.