Mourinho kuwakalisha benchi hawa wawili mchezo ujao, Rashford kuanza
Jose Mourinho amefanya hitimisho lake baada ya kipigo kutoka kwa Man City Jumamosi,
ambapo ametaja nyota wa manchester United atakayeanza mchezo ujao, na wawili watakaoanzia benchi.
Kocha huyo Mreno amemsifia kinda Marcus Rashford aliyeingia kipindi cha pili kwenye mchezo wa Manchester Derby.
"Mchezo mkubwa unaofata ni dhidi ya Feyenoord, na (Rashford) atacheza," Mourinho aliiambia Sky Sports.
"Ninamwamini sana. Ninajua atakua mzuri sana baadaye.
Mourinho pia alifafanua kwanini Jesse Lingard na Henrikh Mkhitaryan wataanzia benchi mchezo ujao dhidi ya Feyernood katika Europa League Alhamisi.
"Siyo kuwaadhibu. Ni namna ambayo ninaweza kuamua perfomance ya timu yangu. Kwa hiyo bila shaka ninaenda kuchezesha wengine."
"Muda mwingine wachezaji wanamvunja moyo meneja. Ni kosa lao au mimi? Vizuri, ni kosa langu kwa sababu mimi ni meneja na ni chaguo langu."
Mourinho kuwakalisha benchi hawa wawili mchezo ujao, Rashford kuanza
Reviewed by Steve
on
Monday, September 12, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, September 12, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment