Propellerads

Arsenal waambulia sare na PSG, Wenger ametoa mtazamo wake





Matokeo: PSG 1-1 Arsenal

Tarehe: 13 September 2016

Uwanja: Parc des Princes


Arsene Wenger amewapongeza wachezaji wake kwa mchezo waliouonesha kupata pointi kwenye mechi ya klabu bingwa dhidi ya Paris-Saint Germain.

The Gunners walizidiwa kwa kiasi kikubwa lakini waliweza kujitetea kwa sare ya 1-1 ugenini, shukrani ziende kwa Alexis Sanchez kwa shambulizi alilofanya zikiwa zimesalia dakika 13 mchezo umalizike.



Edinson Cavani alifunga bao la kuongoza kwa wenyeji mapema kabisa, Wenger amekubali kwamba kikosi chake kilikosa kasi lakini walijitahidi na kuambulia pointi.

"Tulitaka kuanza kwa kasi kubwa lakini ndani ya dakika moja tukawa nyuma kwa 1-0. Ndani ya dakika 20 hatukuwa na kasi, walianza vizuri kuliko sisi lakini tulijikaza," aliwaambia waandishi "Tulicheza vizuri zaidi kipindi cha pili, wao walishuka kidogo.


Arsenal waambulia sare na PSG, Wenger ametoa mtazamo wake Arsenal waambulia sare na PSG, Wenger ametoa mtazamo wake Reviewed by Steve on Wednesday, September 14, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.