Wachezaji wa Manchester United walizinguana chumba cha kubadilishia nguo, kisa!?
Nyota wa Manchester United wameripotiwa kukwaruzana kwenye chumba cha
kubadilishia nguo wakati wa mapumziko kwenye mechi iliyowakutanisha na Manchester City, kabla kocha Jose Mourinho hajazima msala.
Kwa mujibu wa The Sun, baadhi ya wachezaji walitofautiana baada ya kua na mchezo mbaya kipindi cha kwanza.
Inadaiwa Mourinho aliwaacha wachezaji wake kujieleza kwa dakika kadhaa kabla hawajatulia na kujipanga kwa kipindi cha pili.
"Wachezaji walikua wanazozana na kubishana kwa sauti kubwa wenyewe kwa wenyewe. Jose aliamua kuwaacha waongee kwa dakika kadhaa," kiliarifu chanzo kimoja kutoka United kwa gazeti hilo la kiingereza.
Wachezaji wa Manchester United walizinguana chumba cha kubadilishia nguo, kisa!?
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 13, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 13, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment