Propellerads

Ishu ya wachezaji Yanga kuachwa na ndege Algeria, uzembe watajwa




Achana na kipigo cha mabao 4-0 cha juzi Jumamosi kutoka kwa MC Alger, kundi la wachezaji 11 wa Yanga na katibu mkuu wa timu hiyo, Boniface Mkwasa, wamejikuta wakiachwa na ndege baada ya kuchelewa kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Houari Boumediene jijini Algiers, jana.

Taarifa za uhakika kutoka kwa baadhi ya Watanzania waliokuwa wakiisaidia timu hiyo nchini humo zinasema kuwa wachezaji wameachwa na ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki waliyotakiwa kusafiri nayo.

"Nilikuwa miongoni mwa watu tuliofuatana na timu, sasa nadhani kutakuwa kuna uzembe umetokea kwa sababu baada ya mechi walipofika hotelini katibu alikuwa akiwasisitiza wachezaji juu ya suala la kuwahi kufika uwanja wa ndege na aliwatajia muda wa kufika.

"Lakini sasa imekuwaje walichelewa wakati jana (juzi) taarifa ya ya kuwahi na muda ilishatolewa ila cha kushangaza katibu naye yupo katika kundi hilo wakati ndiyo alitoa muongozo huo, wachezaji siwajui majina yao lakini wapo 11.

"Kutokana na hivyo watasubiri hadi Jumatano ili waweze kurudi huko Tanzania kwa sababu ndiyo kutakuwa na ndege ya Shirika la Ndege la Uturuki," alisema Mtanzania huyo.

Yanga baada ya kuondoshwa, wana mchezo wa robo fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prison ambao unatarajiwa kupigwa Aprili 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Ishu ya wachezaji Yanga kuachwa na ndege Algeria, uzembe watajwa Ishu ya wachezaji Yanga kuachwa na ndege Algeria, uzembe watajwa Reviewed by Steve on Monday, April 17, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.