Propellerads

Mesut Ozil anadai Arsenal watakua mabingwa EPL endapo tu...


                               Mesut Ozil                         

Mesut Ozil amesisitiza kua Arsenal wanaweza kuchukua
taji la Premier League.

The Gunners waliwanyuka Man United jumapili iliyopita ambapo wamejikuta wakiachwa kwa point mbili pekee na vinara Man City.

Ozil alifunga kati ya goli moja kati ya matatu ambapo Sanchez alifunga mawili katika kipindi cha dakika 19 za mchezo kuanza.

Sasa nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani anaamini wanaweza kuwa mabingwa endapo kocha Arsene Wenger atakiweka 'fit' kikosi chake.

"Tuna timu kubwa yenye wachezaji wengi World class" Ozil alilialbia gazeti la Ujerumani liitwalo Bild.

"Lengo letu ni kushinda taji la Premier League. Nadhani tunaweza kufikia msimu huu kama tusipopata majeruhi.

"Lakini msimu bado ni mrefu."

Pia huku kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya mambo yakionekana kwenda ndivyo sivyo, huku wakikabiliwa na mechi ngumu ya Bayern Munich, Ozil alisema
"Bila shaka, haitakua rahisi, lakini tuns uwezo wa kuichapa timu yoyote," aliongeza.

"Nikweli tuna pressure kubwa sana kwenye Champions League, lakini tunaweza kuwafunga Bayern, kama tukicheza kwa kiwango kile kile kama kwa Manchester United."






Mesut Ozil anadai Arsenal watakua mabingwa EPL endapo tu... Mesut Ozil anadai Arsenal watakua mabingwa EPL endapo tu... Reviewed by Steve on Thursday, October 08, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.