Propellerads

Stars walivyowanyonga Malawi leo uwanja wa Taifa

                                    Mbwana Samata (kushoto) na Thomas Ulimwengu wakishangilia goli la pili lililofungwa na Ulimwengu


Taifa Stars imeanza vizuri kampeni ya kuwania kucheza Kombe
la Dunia baada ya kuitwanga Malawi kwa mabao 2-0.

                                      Mrisho Ngassa (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa Malawi wakati wa mchezo huo


Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Stars ilipata mabao yake yote mawili katika kipindi cha kwanza.

Bao la kwanza, lilitipiwa kimiani mapema tu na Mbwana Samatta ambaye alikuwa mwepesi kuiwahi pasi maridadi ya Thomas Ulimwengu na kufunga kwa ustadi mkubwa.

Ulimwengu, safari hii akipata ‘zawadi’ kutokana na kumfuatilia kipa wa Malawi aliyeutema mpira wa krosi wa Haji Mwinyi.


                                          Mashabiki waliojitokeza kushuhudia pambano kati ya Stars dhidi ya Malawi huku wakiwa mamebeba bango lenye ujumbe wa kumwamini Mkwasa

Hata hivyo, Malawi walionekana matata zaidi katika kipindi cha kwanza mwanzo wakitawala dakika zote 15 za mwanzo.

Stars ikageuka na kutawala dakika zote za katikati kabla ya wageni kurejea na kutawala kipindi cha pili mwishoni.

Kipindi Kocha Charles Boniface Mkwasa akiwa anaingoza Stars kwa mara ya kwanza akiwa Kocha Mkuu mwenye mkataba, aliwatoa Mrisho Ngassa akamuingiza Salum Telela na Simon Msuva akaingia badala ya Thomas Ulimwengu.

Mchezaji mwingine aliyeingia ni Ibrahim Ajibu na kufufua nguvu ya ushambuliaji ya Stars.

Hata hivyo, katika kipindi cha pili Stars walitoa nafasi nyingi zaidi kwa Malawi kushambulia zaidi.

Stars walivyowanyonga Malawi leo uwanja wa Taifa Stars walivyowanyonga Malawi leo uwanja wa Taifa Reviewed by Steve on Wednesday, October 07, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.