Baba yake Eden Hazard anaamini hili kutoka kwa kocha Mourinho
Baba yake Eden Hazard anaamini kua mwanae anaweza
kufaidika zaidi kama Mourinho atendelea kutomchezeshaa mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea.
Jose Mourinho alimweka benchi kwa mara ya kwanza nyota huyo kwenye mechi ya klabu bungwa ambayo walipoteza kwa 2-1 mbele ya Porto wiki iliyopita.
Lakini Thierry Hazard (Baba yake Hazard) hilo linaonekana kua jamboi jema kwake, kwani annamini mwanae atapata nafasi ya kupumzika kwa ajili ya michuano ya Euro mwakani huko Ufaransa.
Hazard Snr. alisema "Kama akicheza kidogo, atafikia Euro akiwa hajachoka sana.
"Eden amekua anacheza kikosi cha kwanza tangu akiwa na miaka 16. Ni miaka kama sita, Hajawahi kuachwa au kupata jeraha kubwa.
"Unatakiwa kuweka mambo katika mpango. Kila mwaka anaweka malengo na anatengeneza namna ya kuyafikia.
"Binafsi, anajitambua namna ya kuboresha takwimu zake. Juhudi zake zimelalia pale anapojua yupo."
Baba yake Eden Hazard anaamini hili kutoka kwa kocha Mourinho
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 08, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment