Hii hapa inter view aliyofanya Mkwasa na Shaffih Dauda baada ya mechi ya Malawi
Kocha kuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
Charles Boniface Mkwasa amefanikiwa kupata ushindi wa kwanza tangu akabidhiwe mikoba ya kukinoa kikosi hicho. Mkwasa ameiongoza Stars kwenye ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Malawi ikiwa ni mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.
Mtandao wa ShaffihDauda ulifanikiwa kuzungumza na Mkwasa ili kupata tathmini fupi ya mchezo dhidi ya Malawi na malengo ya kocha huyo kuelekea kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa Septemba 11 mwaka huu nchini Malawi.
Shaffihdauda.com: Kikosi cha Stars kilionekana kutengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli zaidi ya yaliyopatikana lakini kimeishia kupata magoli mawili tu, je umeridhika na ushindi huo?
Mkwasa: Nimefarijika na matokeo ya ushindi lakini sijafarijika na idadi ya magoli tuliyoyapata, tulikuwa na uwezo wa kupata magoli mengi zaidi ya mawili.
Lakini tulichokipata tunashukuru kwa Mwenyezi Mungu kwasababu tumefabya attempts nyingi, tumepata nafasi nyingi second half lakini ndio matokeo ya mpira wakati mwingine tunakosea.
Shaffihdauda.com: Tofauti na mechi dhidi ya Nigeria ampapo vijana walionekana wakiwa na stamina na pumzi lakini kwenye mchezo dhidi ya Malawi haikuwa hivyo, nini tatizo?
Mkwasa: Wenzetu wa TP Mazembe walikuwa na mechi kubwa Jumapili na leo Jumatano (jana), wamekuja hapa juzi usiku hata ule muda wa ku-recover walikuwa hawana.
Ukifananisha na mechi ya kwanza ya Nigeria na hii ya Malawi ni vitu viwili tofauti hata game approach ni tofauti pia. Timu zipo tofauti na kila timu inacheza kwa falsafa yake. Na wakati tunaelekea kucheza na Nigeria tulikuwa kambini kwa siku 10 tukifanya intensive training kwahiyo huwezi kuwa na fitness sawa wakati wengine wako kwenye ligi na wengine wako kwenye competition ndio maana hata wakati wa kufanya marking kulikuwa na shida kidogo.
Mechi ilikuwa karibu sana kwasababu walikuwa kwenye ligi kwahiyo huwezi kufanya mazoezi ya kutengeneza staminer kwasababu upo kwenye ligi. Kila mchezaji anapokuja kutoka kwenye timu yake anakuja na level ya fitness ya timu yake. Timu zinatofautia kuna wengine wanakuja wako vizuri na wengine wanakuwa tofauti.
Shaffihdauda.com: Kumekuwa na tatizo la timu ikipoteza mipira inakuwa ni shida kukaba na kuunyang’anya mpira toka kwa wapinzani, utafanya nini kuhakikisha Malawi hawapati nafasi hiyo kwenye mechi ijayo?
Mkwasa: Ni kweli hilo tatizo tunalo si kwa timu ya taifa peke yake, kitaalamu tunasema transitional ni kile kipindi ambacho umekuwa na mpira halafu umepotea sasa ku-react kuutafuta tena kwa mara ya pili. Sasa inakuwa shida kidogo kwasababu hatuna mazoea yale kwenye vilabu vyetu, tunajaribu kuzungumza lakini si rahisi kushika ndani ya siku chache.
Hii hapa inter view aliyofanya Mkwasa na Shaffih Dauda baada ya mechi ya Malawi
Reviewed by Steve
on
Thursday, October 08, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment