Propellerads

Hatari!!, Van Gaal adaiwa kumpuuza Giggs



Kuna madai kua kocha wa Man United, Louis van Gaal
amekua akimpuuza na kutomjali msaidizi wake Ryan Giggs.

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Wim Kieft anaamini kua Van Gaal anatumia zaidi staff wake wa kiholanzi kitu ambacho kilionekana zaidi  kwenye mechi ya klabu bingwa dhidi ya PSV Eindhoven.

Kieft pia ameendelea kuthibitisha kua kitu hicho hicho kilionekana kwenye mechi dhidi ya Barcelona mwanzoni kabisa mwa msimu.

"Hakuna aliyeamini kitu tulichokiona pale United walipocheza na PSV kwenye klabu bingwa." Kieft aliiambia The Mirror

"Luke Shaw alipoumia, walikua na dakika nane za kumuandaa Marcos Rojo kuingia kama Substitute.

"Waliutumiaje huo muda!!, kwanza kabisa Frank Hoek alikuja na rundo la karatasi na kuvaa miwani yake kumsomea maelekezo (Marcos) Rojo.

"Halafu msaidizi mwingine wa Van Gaal,  Albert Stuivenberg akaenda na kumwambia Rojo cha kufanya.
"Na baadaye Van Gaal akafikiria ni bora amuelekeze kwa maneno yake mwenyewe, kwa hiyo ni mtu wa tatu kumuelekeza Rojo namna ya kucheza.

"Ryan Giggs hakuonekana, na miongoni mwa benchi la ufundi la Van Gaal ambaye amecheza mechi nyingi kwa kiwango kikubwa kuliko makocha wengine na ana uzoefu mkubwa.

"Inaonekana Van Gaal anategemea zaidi staff wa kidachi- na wote tuliona matatizo yaliyotokea alipofanya kitu kama hicho mechi ya Barcelona"



Hatari!!, Van Gaal adaiwa kumpuuza Giggs Hatari!!, Van Gaal adaiwa kumpuuza Giggs Reviewed by Steve on Sunday, September 20, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.