Propellerads

Kufuatia majeraha ya Luke Shaw, Man United sasa kumnasa huyu mbele ya Chelsea na Man City




Kocha Louis Van Gaal ana mpango wa kumnasa beki wa kushoto
wa West Ham,  Aaron Cresswell kufuatia kuumia kwa Luke Shaw.

Shaw atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi isiyopungua sita kutokana na kuvunjika mguu wake wiki iliyopita kwenye mechi ya klabu bingwa dhidi ya PSV Eindhoven.

Na kwa mujibu wa The Sun, Red Devils wanajipanga kutenga dau la  £15million kwa Cresswell kipindi dirisha la usajili likifunguliwa tena Ulaya Januari mwakani.

Beki huyo pia anadaiwa kuwa katika mipango ya vilabu vingine vya Premier League ambavyo ni Man City na Chelsea.

Lakini Van Gaal amesema kua itakua ni ngumu kuziba pengo la Shaw kutokana na mwanzo mzuri aliouonesha msimu huu.

"Kwetu ni hasara kubwa, kwa sababu kama nilivyosema mwanzoni kua huu ulikua ni msimu wa Luke Shaw, na inaonekana kama tayri ushaisha" alisema bosi huyo wa Old Trafford.

"Tulitengeneza wing ya kushoto tukiwa na Memphis Depay na Luke Shaw, na sasa tunatakiwa kutengeneza tena kwa sababu tunatakiwa kupambana na hili tatizo"
z



Kufuatia majeraha ya Luke Shaw, Man United sasa kumnasa huyu mbele ya Chelsea na Man City Kufuatia majeraha ya Luke Shaw, Man United sasa kumnasa huyu mbele ya Chelsea na Man City Reviewed by Steve on Sunday, September 20, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.