Balaa la Tambwe na Ngoma ligi kuu Vodacom ni noma, mpaka sasa wana idadi hii ya magoli
Washambuliaji wa kigeni, Donald Ngoma na Amis Tambwe
wameendelea ‘kuwatesa makipa’ wa ligi kuu bara baada ya kila mmoja kufunga katika mchezo wa ushindi dhidi ya JKT Ruvu jioni ya katika uwanja wa Taifa. Yanga imeshinda kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu.
Mzimbabwe, Ngoma alifunga goli lake la tatu katika gemu tatu za ligi kuu dakika ya 33′. Ngoma alifunga akiwa ndani ya eneo la hatari akimalizia’ kiulaini’ pasi ya kisigino iliyopigwa na Tambwe. Hilo lilikuwa goli la tatu kwa mshambulizi huyo aliyesajiliwa kutoka FC Platinum ya kwao Zimbabwe, awali alifunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union siku ya ufunguzi, kisha akafunga moja ya magoli matatu ya Yanga katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Tambwe alifunga magoli 19 msimu wake wa kwanza akiwa mchezaji wa Simba SC na kushinda tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2013/14, akafunga mara 15 msimu uliopita alipomaliza kama mfungaji namba mbili akiwa na kikosi cha Yanga. Amefunga mara mbili dhidi ya JKT Ruvu na hivyo kufikisha jumla ya magoli matatu katika michezo mitatu msimu huu.
Alifunga goli lake la kwanza akimalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa JKT Ruvu, Tonny Kavishe kufuatia ‘krosi kick’ ya winga Deus Kaseke dakika tatu tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, akafunga kwa ‘stahili yake’ baada ya kuunganisha krosi ya Saimon Msuva.
Wakizugukwa na viungo wa pemnbeni wenye kasi, Msuva na Kaseke huku wakipata pasi nzuri kutoka kwa viungo wa kati, Mnyarwanda, Haruna Niyozima na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko washambuaji hao wataendelea kufunga msimu huu kutokana na umakini walio nao. Kufunga magoli 6 kati ya 9 ya timu yao katika michezo mitatu ni dalili njema kuwa Yanga imepatia kuwasaini.
Malimi Busungu aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya Ngoma dakika ya 86’ lakini alipoteza nafasi ya wazi zaidi katika mchezo dakika mbili baada ya kuingia uwanjani. Hakuwa makini licha ya kuusoma mchezo kwa dakika 86’ akiwa katika benchi. Ameoesha tofauti yake na washambuaji hao wa Kigeni.
Balaa la Tambwe na Ngoma ligi kuu Vodacom ni noma, mpaka sasa wana idadi hii ya magoli
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 20, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, September 20, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment