Xavi afunguka kwa nini Ronaldo hakustahili Ballon d'Or.
Aliyekua kapteni wa FC Barcelona, mkongwe Xavi Hernandez amefunguka kwa nini Cristiano Ronaldo hakustahili kabisa
tuzo ya mwanasoka bora duniani ( Ballon d'Or) mwaka jana 2014.
Xavi afunguka nani anaweza kua mkali wa dunia baada ya Messi.
Mchezaji huyo aliyeondoka Barca kuelekea klabu ya Al Sadd, ameongea hayo alipokua akizungumzia mabishano ya muda mrefu kua kati ya Ronaldo na Messi nani mkali.
"Kama ukitoa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi daima atachukua tu" aliiambia Sport.
"Kama kuna mwaka wa mpira kwake, aling'aa 2010, ya mwaka jana alitakiwa achukue mjerumani.
"kwa nini Ronaldo alishinda wakati mabingwa wa dunia walikua ni Ujerumani?"
Xavi alisistiza kua hata kama Ballon d'Or ikitolewa hata sasa hivi, Messi anastahili kuchukua, ambapo Ronaldo anasifiwa kuonekana bora na wachezaji wenzake tu.
"Kama tukipiga kura kupata mchezaji bora lazima atakua Messi, yeyote atakaesema tofauti labda wataku ni timu moja na Ronaldo" aliongeza.
"Mtu yeyote anaejua mpira vizuri, anaweza kuona kua Messi ndiye bora kuanzia uchezaji binafsi na pia kama timu"
Xavi afunguka kwa nini Ronaldo hakustahili Ballon d'Or.
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
