Tetesi: Man United wamtengea pauni 18 mil. mbrazil huyu.
Kituo jimoja cha redio nchini Uingereza kinachoitwa Talksport kimedai kua Man U wanamfukuzia kiungo huyo wa Hoffenheim.
Mkali huyo kwa sasa yupo Chile na kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, huku akidaiwa kuuvutia uongozi wa Man United katika perfomance yake kuanzia katika klabu anayochezea hadi timu ya taifa.
"Firmino amekua ni mtiifu sana Hoffenheim, ila amewashangaza wengi baada ya kukataa kusaini mkataba mpya mwezi machi" mchambuzi wa ligi ya Ujerumani Bundesliga aliiambia Talksport.
"Anahisi klabu ndio imemfanya akue, lakini baada ya kushindwa kufuzu kwa ajili ya michuano ya Ulaya, inaonekana ni muda sahihi wa kuodoka.
Amekua kwenye rada za Man United kwa muda mrefu, na amewavutia kutokana na uwezo wake wa kuto mchango mkubwa kwa timu.
"Kama Man U watampata, watakua wamefanya la maana sana"
Hata hivyo, haijalishi kama mazungumzo yanafanyika na Man U au la, lakini mkali huyo ataondoka klabuni kwake mara tu baada ya michuano ya Copa America.
Firmino amefunga magoli 11 msimu huu na kutoa usaidizi mara 10.
Tetesi: Man United wamtengea pauni 18 mil. mbrazil huyu.
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, June 12, 2015
Rating:
