Propellerads

Mourinho amtaka Pogba kwa Oscar.




Kocha wa Chelsea, Jose Chelsea anadaiwa kua tayari kummuza mchezaji wake Oscar kwa Juventus, ila tu kama nao watakubali kumuuzia
Paul Pogba.

Mourinho anaungana na vilabu vingi vikubwa Ulaya vilivyoonesha nia ya kumtaka nyota huyo kutoka Ufaransa.

Juventus wanadaiwa kuonesha kuvutiwa na Oscar, hivyo wanataka kumuingiza kikosini mwao.

Zapsportz imeripoti kua kuna uwezekano mkubwa vilabu vyote viwili kukutana na kuzungumzia swala hilo, lakini uamuzi mkubwa utabaki kwa wachezaji kama kila mmoja atakubali uhamisho huo.

Manchester City, Barcelona na Real Madrid ni miongoni mwa timu zilizoonesha nia ya kumpata Pogba, huku Man City wakimtangaza kumtengea dau la pauni mil. 80.

Oscar kwa sas anaonekana kutopata nafasi ya kutosha Stamford Bridge, na anaweza kuondoka ili kupata sehemu nyingine ambayo atapata nafasi ya kutosha.

Vyombo vya habari nchini Italia vimeripoti kua Juventus wameonesha nia kubwa ya kumtaka Oscar, huku Mourinho akitaka kutumia mwanya huo kumpata Pogba.
Mourinho amtaka Pogba kwa Oscar. Mourinho amtaka Pogba kwa Oscar. Reviewed by Steve on Friday, June 12, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.