Propellerads

Xavi afunguka kua ni nani rafiki yake mkubwa Catalan.




Kiungo mkongwe wa FC Barcelona, Xavi Hernandez amefunguka kua ni nani ambaye ni rafiki yake mkubwa katika
 chumba cha kubadilishia nguo Catalan.

Xavi mwenye miaka 35, anaweza kuelekea katika klabu yake mpya Al Sadd Alhamisi hii, huku kiungo Sergio Busquets akiwa ni mrithi wake katika klabu.

Xavi anasema Busquets ni "rafiki wa karibu" ndani na nje ya uwanja na anaona kama yeye baadaye  atakua  nahodha.wa Barca

"Mimi nimepata mchango mkubwa wa Busquets katika kila heshima," Xavi aliiambia tovuti rasmi ya UEFA .

"Yeye ni rafiki wa karibu na nadhani yeye ni mchezaji mwenye uelewa mkubwa zaidi duniani wa mpira wa miguu, katika ushambuliaji  na katika ulinzi.

"Anacheza kwa akili na kustaajabisha uwanjani.

"Na mbali na yeye, sioni mwingine wa kumlinganisha nae.

"Nadhani yeye ni mbadala wangu  katika chumba cha kubadilishia nguo na uwanjani.

"Anastahili kua kiongozi wa Barca katika miongo ijayo, bila shaka wala wasi."

Xavi afunguka kua ni nani rafiki yake mkubwa Catalan. Xavi afunguka kua  ni nani rafiki yake mkubwa Catalan. Reviewed by Steve on Thursday, June 11, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.