TFF yaruhusu idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwa vilabu.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limepitisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni watakaosajiliwa.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine amesema wamepitisha hilo baada ya kamati ya utendaji ya shirikisho hilo iliyokaa leo mjini Zanzibar.
“Wachezaji wasizidi saba, lakini pia wote saba wanaruhusiwa kucheza kama timu itaamua kuwatumia,” alisema.
Kabla ya hapo timu moja ilikuwa inaruhusiwa wachezaji wasiozidi watano baada ya TFF kupunguza kutoka kumi.
TFF yaruhusu idadi ya wachezaji saba wa kigeni kwa vilabu.
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 20, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 20, 2015
Rating:
