Hazard ataja wakongwe wawili waafrika anaowaheshimu.
Nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard, ametaja nyota wawili wakongwe anaowaheshimu ambao kwa
namna moja au nyingine walimuonesha msaada katika chumba cha kubadilishia nguo Stamford Bridge katika misimu miwili iliyopita.
Winga huyo mbelgiji alionesha kiwango kizuri na The Blues msimu uliopita, hivyo kuisaidia timu yake kuchukua ubingwa wa EPL na kombe la Capital one.
Hazard ambaye alichukua uchezaji bora PFA 2015, amewataja waliokua washambuliaji wa Chelsea, Didier Drogba na Samuel Eto'o kwa mchango waliokua nao kwake.
"Kwangu Drogba alifanya makubwa kama Samuel Eto'o msimu uliopita, mkongwe ambaye unaweza kumpa heshima sana" aliuambia mtandao wa Standard.co.uk.
"Niliweza kuongea nao mara nyingi kwa sababu wanazungumza lugha moja na mimi"
"Labda ukweli ni kwamba katika chumba cha kubadili nguo, alitusaidia sana, na mchango wa kila mtu una nafasi kubwa.
"Ninajivunia kua, ninaweza kuwaambia watoto wangu kua nilicheza nae na tulichukua ubingwa pamoja, nina huzuni kwa kua ameondoka, lakini tunawasiliana kila siku, ni mkongwe na ninamheshimu sana"
Eto'o alicheza msimu mmoja Stamford Bridge, huku Drogba alondoka tena Chelsea kwa mara nyingine msimu ulioisha wa 2014/15 .
Hazard ataja wakongwe wawili waafrika anaowaheshimu.
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 20, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, June 20, 2015
Rating:
