Propellerads

Liverpool nao wamfukuzia Firmino anaefukuziwa na Man United.




Klabu ya Liverpool wanadaiwa kumfukuzia nyota wa Hoffenheim , Firmino, ambae siku za hivi karibuni Man United nao waliripotiwa kumuwinda.

Liverpool kwa sasa wanaangalia uwezekano wa kumnasa nyota huyo, lakini hawako tayari kungoja mpaka nyota wao Raheem Sterling aondoke. Anfield tayari wameshakataa ofa mbili za Man City kwa Sterling, huku wakisisitiza City lazima watoe pauni mil 50 kumpata Sterling.

Firmino kwa sasa yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Brazil katika michuano ya Copa America huko Chile, alidaiwa pia kuwindwa na kocha Louis van Gaal.

Kiungo huyo amekua 'hot' kwa sasa huko Ulaya kutokana na kiwango alichoonesha akiwa na klabu yake ya Heffenheim msimu uliopita.

Inadaiwa kwa sasa uhamisho wa nyota huyu unaweza kua na thamani ya pauni mil. 13 hadi 15.
Liverpool nao wamfukuzia Firmino anaefukuziwa na Man United. Liverpool nao wamfukuzia Firmino anaefukuziwa na Man United. Reviewed by Steve on Saturday, June 20, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.