Propellerads

Kumbe Memphis Depay wa Man United ni mkali wa 'free-kick' kuliko Messi na CR7.




Huku Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wakionekana ni mafundi zaidi uwanjani, lakini imebainika nyota mpya wa Man United aliyesajiliwa msimu huu anawazidi kwa
ufungaji wa free kick  ,hata kama mabao yao yote waliyofunga kwa free kick msimu uliopita yakichanganywa.

Depay aliyesajiliwa na Man United kipindi hiki cha usajili kwa dau la pauni mil. 25, amefunga jumla ya magoli saba kwa mashuti ya free kick msimu uliopita akiwa PSV.

Ronaldo na Messi wao wamefunga jumla ya magoli mawili pekee kila mmoja kwa free kick La liga msimu ulioisha, pia Memphis ana wastani mzuri katika free kick kuliko mastaa hao.

Nyota huyo alifunga jumla ya mabao 7 katika free kick attempts 33 alizofanya, ukiwa ni wastani wa asilimia 22.21, huku Ronaldo akiwa na magoli mawili pekee kwa majaribio mengi ya mashuti aliyopiga ikileta wastani wa asilimia 6.06.

Messi nae alipiga jumla ya free kick 37 huku akifunga magoli mawili pekee, ukiwa ni wastani wa asilimia 5.41.

Hata hivyo Depay
pamoja na rekodi hiyo, nae anazidiwa na mkali kutoka Werder Bremen, Zlatko Junuzovic ambae amefunga jumla ya magoli 5 katika free kicks 22 tu alizopiga- katika kiwangoi cha asilimia 22.73.



Depay ambae ujio wake Man United unafananishwa na Cristiano Ronaldo, ni miongoni mwa wachezaji 17 katika ligi kubwa za Ulaya wenye wastani mzuri katika ufungaji wa free kick, hii ni kulingana na mujibu wa utafiti

Kumbe Memphis Depay wa Man United ni mkali wa 'free-kick' kuliko Messi na CR7. Kumbe Memphis Depay wa Man United ni mkali wa 'free-kick' kuliko Messi na CR7. Reviewed by Steve on Saturday, June 20, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.