Petr Cech asema dili na Arsenal halijakamilika.
Petr Cech amekanusha na kusema kwamba dili lake kujiunga Arsenal halijakamilika kama
ilivyoripotiwa.
Raia huyo wa Czech anatizamiwa kua na uelekeo mkubwa wa kujiunga The Gunners, huku baadhi ya ripoti zikidai dili hilo lenye thamani ya pauni mil 11 limeshafikiwa tayari.
Hata hivyo kupitia ukurasa wa Twitter wa uongozi wa kampuni inayomsimamia , mkali huyo amekanusha ripoti hizo, Tweet hiyo ilisomeka hivi; "No transfer deal has been done yet for @PetrCech - as soon as any news @PetrCech will confirm"...ukimaanisha kua hakuna dili yeyote iliyofanyika mpaka Cech mwenyewe atakapothibitisha.
Cech mwenye miaka 33 kwa sasa amekua Chelsea kwa miaka 11, lakini amepata nafasi kidogo sana ya kukichezea kikosi cha The Blues msimu uliopita mara baada tu ya kurejea kwa Thibaut Courtois ambaye ndiye kipa namba moja sasa Chelsea akitokea Atletico Madrid alikokua kwa mkopo alikokua kwa vipindi vitatu.
Petr Cech asema dili na Arsenal halijakamilika.
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 23, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, June 23, 2015
Rating:
