Propellerads

Sababu tano, kwanini Ronaldo anataka kuondoka Real Madrid.




Nyota Cristiano Ronaldo kipindi hiki cha usajili amekua akihusishwa kwa kiasi kikubwa kutaka kuhama Real Madrid, huku sababu kubwa ikidaiwa kua ni
matatizo katika uongozi klabuni hapo. Hapa nimekuletea sababu tano kwanini anataka kuondoka;

Kwa mujibu wa chapisho moja la kihispania, AS,  swala la kwanza linaanzia pale Ronaldo alipofanya party yake ya siku ya kuzaliwa 'birthday'. Ronaldo anaona kua klabu haikumlinda wakati wa mabishano makali yaliyotokea kwenye party yake.

Sababu ya pili ni kua, Ronaldo anashangazwa na jinsi uongozi wa klabu unavyowafanyia nyota wakongwe kama vile Iker Casillas na Sergio Ramos, anaamini ni kama klabu haithamini wakongwe wake, hivyo hata yeye ana hofu kua siku moja anaweza fanyiwa hivyo.

Pia imefahamika kua kuna kutokuelewana kati ya wachezaji na mkuu wa kitengo cha matibabu, Jesus Olmo, wachezaji hawafurahishwi na jinsi wanavyotibiwa wakiumia, huku tayari klabu imeshatangaza mkataba mpya na mtu huyo.

Kitu kingine kilichomo katika mawazo ya Ronaldo ni kua, anatarajiwa kupangwa kucheza nafasi nyingine msimu ujao, na swala hili kasikia kwenye vyombo vya habari pekee, huku kukiwa hapana mazungumzo yoyote yaliyofanywa kwake.

Na mwisho ni kua, Ronaldo hajafurahia kitendo cha kocha mpya, Rafael Benitez, cha kukutana na Gareth Bale na kuzungumzia mambo ya baadae, huku yeye hajafanyiwa mazungumzo yoyote.

Ronaldo kwa sasa anawindwa na klabu yake ya zamani, Manchester United, na kama hali ya sasa itaendelea kua mbaya, huenda akarejea Old Trafford.
Sababu tano, kwanini Ronaldo anataka kuondoka Real Madrid. Sababu tano, kwanini Ronaldo anataka kuondoka Real Madrid. Reviewed by Steve on Tuesday, June 23, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.