Propellerads

Hans Poppe afunguka kuhusu pesa za Kessy kusaidia kukomboa nyasi za Simba bandarini, ukweli upo hivi...




Uongozi wa Klabu ya Simba umeweka bayana kwamba miongoni mwa fedha ambazo wamezitoa kuzilipia nyasi zao zilizokwama bandarini ni zile walizopata kutoka kwa wapinzani wao Yanga kupitia kwa beki wao, Hassan Kessy.

Yanga walilazimishwa kuwalipa Simba kiasi cha shilingi milioni 50 kufuatia kubainika kwamba walimsajili beki huyo kinyume na utaratibu mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba.

Ikumbukwe kuwa, Simba ililazimishwa kuzikomboa nyasi zao bandia ambazo zitaenda kuwekwa katika uwanja wao wa Bunju uliopo jijini Dar, zilizokwama bandarini kutokana na kushindwa kulipiwa kodi ambapo Mmlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliweka hadharani kuzipiga mnada endapo wangeshindwa kuzilipia.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Poppe, amefunguka kwamba kuwa tayari wameshalipa kiasi wanachodaiwa Sh milioni 83 za kodi.

"Sisi tumeshamalizana na TRA na tushachukua kilicho chetu kwa kuwapa fedha ambazo walikuwa wanatudai Sh milioni 83, na kilichobakia kwa sasa ni kuufuata mzigo wetu na kuendelea na harakati za ujenzi wa uwanja wetu.

"Pia katika fedha hizo tulizozitoa kuna fedha tulizipokea kutoka kwa watani zetu Yanga ambazo zilitokana na mauzo ya Kessy ambazo zimetusaidia katika kuzikomboa nyasi hizo na sehemu nyingine tulichangishana wenyewe," alisema Hans Poppe.


Hans Poppe afunguka kuhusu pesa za Kessy kusaidia kukomboa nyasi za Simba bandarini, ukweli upo hivi... Hans Poppe afunguka kuhusu pesa za Kessy kusaidia kukomboa nyasi za Simba bandarini, ukweli upo hivi... Reviewed by Steve on Friday, April 07, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.