Propellerads

Kocha Mbao FC atamba kutumia siri aliyoiona kwa Kagera Sugar kuimaliza Simba namna hii




Kocha mkuu wa Mbao FC, Etienne Ndayiragije, amesema ameisoma Simba katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar na kufahamu udhaifu wao.

Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kupoteza kwa mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Ndayiragije amesema anatarajia kutumia udhaifu wa wachezaji wa Simba aliounona kuibuka na ushindi kwenye mechi yao itkayochezwa Jumatatu wiki ijayo katika Uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.

"Simba nawajua nilicheza nao mzunguko wa kwanza, pia katika mchezo wao uliopita dhidi ya Kagera Sugar nimeona jinsi wanavyocheza na nimechukua vitu vya kufanyia kazi, hivyo sina ninachohofia," alisema Ndayiragije.

Kocha huyo ambaye pia amewahi kumfundisha straika wa Simba, Laudit Mavugo, alisema hana presha na mchezo huo kwani anachukulia wa kawaida kwake.

"Mchezo wetu na Simba ninaona utakuwa wa kawaida tu kama ilivyo mingine ya Ligi Kuu tuliyocheza na kama wametoka kufungwa hata sisi tutawafunga, Nakiamini kikosi changu na maandalizi yanaendelea zaidi nikifanyia kazi kile nilichokiona kwa Simba walipocheza na Kagera."
Kocha Mbao FC atamba kutumia siri aliyoiona kwa Kagera Sugar kuimaliza Simba namna hii Kocha Mbao FC atamba kutumia siri aliyoiona kwa Kagera Sugar kuimaliza Simba namna hii Reviewed by Steve on Thursday, April 06, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.