Propellerads

Hivi ndivyo Simba walivyomaliza suala la nyasi zao bandarini, achana na tetesi




Klabu ya Simba imefanikiwa kulipia kodi nyasi bandia 'kapeti' zilizokwama Bandari ya Dar es salaam baada ya kuletwa nchini.

Simba imelipa Sh milioni 80 baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutaka kuzipiga mnada nyasi hizo kutokana na kukaa kwa muda mrefu bandarini bila kulipia kodi.

Nyasi hizo sasa zitatandikwa kwenye uwanja wao ulioko Bunju nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, ambao sasa utatumika kwa mazoezi na mashindano mbalimbali.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo, jana alithibitisha kuwa Simba wamefanikiwa kulipa kiasi walichokuwa wanadaiwa.

Kayombo alisema viongozi wa klabu hiyo ya Simba walipewa siku 14 kuhakikisha wamelipa kiasi walichokua wakidaiwa kabla ya kuzipiga mnada.


Hivi ndivyo Simba walivyomaliza suala la nyasi zao bandarini, achana na tetesi Hivi ndivyo Simba walivyomaliza suala la nyasi zao bandarini, achana na tetesi Reviewed by Steve on Thursday, April 06, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.