Propellerads

Huyu hapa Omog akimchambua Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar




Kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog, raia wa Cameroon ameibuka na kumchambua straika Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar kwa kusema kuwa mshambuliaji huyo ni hatari kwani aliweza kuichachafya ngome yake iliyokuwa mikononi mwa Mganda, Juuko Murshid.

Akimzungumzia mshambuliaji huyo, Omog amesema kwamba Mbaraka ni miongoni mwa mastraika hatari kwa sasa na hilo linadhihirishwa na kiwango chake cha kufunga mabao lakini pia kutoogopa mabeki na upambanaji.

"Ni mshambuliaji mzuri na anayejua kufunga, nimpongeze juu ya hilo lakini  pia nimebaini kwamba ana kiu ya kupambana na haogopi beki yeyote yule na katika mechi yetu na wao yeye pamoja na kina Juma Kaseja ndio waliotubania kuibuka na pointi tatu.

"Utaona kipaji chake kwa jinsi alivyoivuruga beki yetu ambayo ina wachezaji wazuri lakini walimshindwa na alitufunga, jambo ambalo naweza kusema kwamba ni mchezaji hatari na kama akiendelea kudumu katika kiwango chake atafika mbali," alisema.
Huyu hapa Omog akimchambua Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar Huyu hapa Omog akimchambua Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar Reviewed by Steve on Wednesday, April 05, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.