Hatimaye sababu ya Ulimwengu kutimka Mazembe yawa wazi
Imebainika kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga AFC Eskilstuna ya Sweden, Thomas Ulimwengu, alilazimika kuihama TP Mazembe ya DRC baada ya klabu hiyo kuvunja ghafla mkataba wake.
Inadaiwa Mazembe walifikia uamuzi wa kuvunja mkataba wa Ulimwengu baada ya mchezaji huyo kupata majeraha yaliyotishia kumweka nje kwa kipindi kirefu.
Chanzo kutoka DRC kimefunguka kwamba uamuzi huo usio wa kiuungwana wa kuvunja mkataba wa Ulimwengu, ulienda sambamba na kumlipa stahiki zake zote na kumtaka aondoke mara moja katika klabu hiyo.
"Yaani unajua jamaa ni watu wabaya sana, Ulimwengu alikuwa bado ana mkataba na Mazembe lakini kulitokea figisu figisu za ghafla na jamaa wakaamua kukatisha mkataba wake na kumlipa stahiki zake zote, yaani hawakujali mazuri yote aliyowafanyia," kilieleza chanzo cha habari.
Inadaiwa kitendo hicho kilimweka katika wakati mgumu mshambuliaji huyo ambaye kipindi hicho alikuwa akisumbuliwa na majeraha.
"Unajua jamaa walijua hataweza tena kupona na kucheza ndio maana wakafanya maamuzi magumu." kiliongeza chanzo hicho.
Hata hivyo Ulimwengu mwenyewe hakupatikana kuzungumzia ishu hiyo.
Hatimaye sababu ya Ulimwengu kutimka Mazembe yawa wazi
Reviewed by Steve
on
Tuesday, March 28, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment