Aliyekuwa katibu mkuu Yanga atoa nasaha kwa viongozi wa klabu juu ya hali ya sasa
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha, amesema kutowajibika ipasavyo kwa uongozi wa klabu hiyo ndiyo chanzo cha mabingwa hao watetezi Ligi Kuu tanzania Bara kuondolea Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tiboroha amesema viongozi wa klabu hiyo hawakutimiza ipasavyo majukumu yao hatua iliyosababisha waondolewe mapema kwenye michuano hiyo.
"Huu ni wakati wa kuangalia uongozi ulijikwaa wapi na kujirekebisha mapema, ili timu iweze kufanya vizuri katika michezo yao ijayo ya kimataifa na ligi kwa ujumla," alisema Tiboroha.
Pia kuhusu wigo mdogo wa wachezaji,amefunguka na kudai ni tatizo kubwa kwa timu nyingi za Ligi Kuu Tanzania Bara jambo linalopelekea mchezaji mmoja au wawili wasipokuwapo basi timu nzima inapoteza mwelekeo,
"Mfano Yanga wakati wanashiriki michuano hiyo wachezaji wengi walikuwa na majeraha, hili nalo lilichangia kwa kiasi kikubwa kutopata matokeo mazuri kwenye mechi yao na Zanaco," alisema.
Aliyekuwa katibu mkuu Yanga atoa nasaha kwa viongozi wa klabu juu ya hali ya sasa
Reviewed by Steve
on
Tuesday, March 28, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment