Kuelekea mchezo na Azam FC, Cannavaro anawatoa hofu mashabiki wa Yanga namna hii...
Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro', amesema anafahamu ukubwa wa vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakati huu kati yao na Simba, hivyo kikosi chao kitapambana kwa nguvu kuhakikisha kinailaza Azam.
Yanga na Azam zitashuka dimbani wikiendi hii kuumana katika pambano la ligi hiyo litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza jana, Cannavaro amesema anafahamu ugumu wa mechi wanapokutana na Azam lakini akawataka mashabiki wa klabu hiyo waondoe shaka akidai kikosi chao kimepikwa kikaiva tayari kwa mchezo huo.
"Hakuna tofauti kati ya timu hizi, sisi ni wazuri kama ilivyo Azam, mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunapata pointi tatu ili tukalie kiti cha uongozi.
"Nawaomba mashabiki wasikatishwe tamaa na chochote, wajitokeze uwanjani Aprili mosi kutuunga mkono kwa kuwa tupo kwenye mapambano kuwania ubingwa na wapinzani wetu Simba na tukishinda dhidi ya Azam tutakuwa pazuri," alisema.
Kuelekea mchezo na Azam FC, Cannavaro anawatoa hofu mashabiki wa Yanga namna hii...
Reviewed by Steve
on
Tuesday, March 28, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment