Sanchez kutimkia Bayern Munich, Barca nao wanakomaa na Coutinho....hizi hapa stori zilizobamba magazeti ya Ulaya leo Jumanne
Alexis Sanchez ni miongoni mwa wachezaji wawili wakubwa ambao wapo katika rada za Bayern Munich kuelekea usajili majira ya joto.
Inadaiwa kwamba mabingwa hao wa Ujerumani wapo tayari kuwapa mikataba Alexis Sanchez na nyota mwingine kutoka Real Madrid, James Rodriguez ambaye bosi wa sasa wa Bayern, Carlo Ancelloti alimsajili mwka 2014 alipokua akiinoa Real.
Mkataba wa sasa wa Sanchez na Arsenal unafikia tamati mwishoni mwa msimu ujao ambapo Gunners huenda wakalazimika kumuuza majira ya joto ili kutokuja kumpoteza bure.
Stori kubwa leo kutoka magazeti ya Ulaya Jumanne hii
- Real Madrid bado wanamtaka Eden Hazard huku klabu ya sasa ya Mbelgiji huyo Chelsea wakikataa kukanusha wala kukubali kupata ofa kutoka kwa vigogo hao wa Hispania.
- Southampton wanaanda dau la pauni mil 20 kwa ajili ya nyota wa Liverpool, Mamadou Sakho.
- Winga wa Manchester City, Jesus Navas bado ni 'target' kubwa kwa Sevilla kuelekea kipindi cha usajili.
- Barcelona wanaweza kumtoa kwa ofa Ivan Rakitic kwenda Liverpool ikiwa ni katika mpango wa kuinasa saini ya Philippe Coutinho.
- Kinda wa Monaco, Tiemoue Bakayoko alikataa uhamisho wa kuelekea Arsenal mwaka jana.
- Arsenal wanataka kumsajili Rui Patricio ambaye ni mlinda mlango wa Sporting Lisbon kama mbadala wa Petr Cech.
Sanchez kutimkia Bayern Munich, Barca nao wanakomaa na Coutinho....hizi hapa stori zilizobamba magazeti ya Ulaya leo Jumanne
Reviewed by Steve
on
Tuesday, March 28, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment